8 Novemba 2020 - 21:08
Rais Rouhani: Hata wananchi wa Marekani hawakusalimika na madhara ya siasa mbovu za Trump

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amegusia matokeo ya uchaguzi wa rais nchini Marekani na kusema kuwa, madhara ya siasa mbovu na Donald Trump hayakuwafika wananchi wa mataifa mengine tu, bali hata wananchi wa Marekani hawakusalimika na madhara ya siasa hizo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Rais Rouhani amesema hayo leo Jumapili katika kikao cha Kamati ya Uratibu wa Kiuchumi ya Serikali na kuongeza kuwa, sasa hivi kumejitokeza fursa kwa serikali ijayo ya Marekani kurekebisha na kufidia yaliyovurugwa na Donald Trump, kuheshimu sheria za kimataifa na kushikamana na mikataba na makubaliano ya kimataifa.

Amesema, daima Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikiheshimu ahadi zake kila pale upande wa pili unapoheshimu ahadi hizo na kwamba kushirikiana na kuwa na uhusiano mzuri na nchi nyingine duniani ndiyo stratijia ya Jamhuri ya Kiislamu.

Rais Hassan Rouhani aidha amesema, muqawama wa wananchi wa Iran umeshinda katika vita vya kiuchumi vilivyoanzishwa na Marekani na kuongeza kuwa, kutokana na muqawama wao wa kishujaa mbele ya vita hivyo vya kiuchumi vya Marekani, taifa la Iran limewathibitishia walimwengu kuwa siasa za mashinikizo na vikwazo vya kiwango cha juu kabisa vilivyowekwa na Washington dhidi ya taifa hili la Kiislamu, zimeshindwa.

Amesema, wakati umefika kwa nchi jirani na Iran kuitikia kwa busara mwito wa ushirikiano wa kuishi pamoja na salama na amani unaotolewa na Jamhuri ya Kiislamu. Vile vile amesema, sasa ni wakati wa kuongeza juhudi za kujenga uchumi thabiti humu nchini. 

342/